logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uganda: Kizza Basigye asusia chakula kushinikiza aachiliwe

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ameanza mgomo wa kula wakati akikaribia miezi mitatu kizuizini akisubiri kesi yake kujadiliwa.

image
na Japheth Nyongesa

Kimataifa13 February 2025 - 15:39

Muhtasari


  • Msaidizi wa vuguvugu lake la kisiasa, People's Front for Freedom (PFF), alisema kuwa Besigye anapinga kifungo chake kinachoendelea, akiamini kuwa anapaswa kuwa nyumbani badala ya kuwa gerezani.
  • Rais Museveni, hata hivyo, ameelezea kusikitishwa na uamuzi huo, akiutaja kuwa si sahihi na kuahidi kuupinga katika mahakama ingine.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ameanza mgomo wa kula  wakati akikaribia miezi mitatu kizuizini akisubiri kesi yake kujadiliwa.

Besigye mwenye umri wa miaka 68, anakabiliwa na mashtaka ya kumiliki bastola na kujaribu kununua silaha nje ya nchi, tuhuma ambazo amekanusha vikali. Kesi yake, ambayo awali iliahirishwa hadi Januari, bado haijapangwa tarehe ya kusikizwa, na hivyo kuchochea maandamano yake.

Msaidizi wa vuguvugu lake la kisiasa, People's Front for Freedom (PFF), alisema kuwa Besigye anapinga kifungo chake kinachoendelea, akiamini kuwa anapaswa kuwa nyumbani badala ya kuwa gerezani.

Besigye, ambaye aliwahi kuwa daktari wa binafsi kwa Rais wa Uganda ambaye amehudumu kwa muda mrefu Yoweri Museveni, amekuwa kiongozi maarufu wa upinzani kwa miaka mingi.

Licha ya kushindwa katika uchaguzi wa urais mara nne dhidi ya Museveni, Besigye ameishutumu serikali kwa mateso ya kisiasa. Shughuli zake za kisiasa zimefifia katika miaka ya hivi karibuni, na hakugombea uchaguzi wa 2021.

Hata hivyo, utekaji nyara wake wa hivi karibuni hapa nchini Kenya na baadaye kulazimishwa kurudi Uganda ulizua malalamiko makubwa ya kimataifa na kuibua wasiwasi juu ya uwezekano wa kubadilishana taarifa za kijasusi kati ya nchi hizi mbili.

Vita vya kisheria vinavyomzunguka Besigye vinapondelea, uamuzi wa Mahakama Kuu ya Uganda mwezi uliopita kwamba mahakama za kijeshi haziwezi kusikiliza na kutoa uamuzi kwa raia na badala yake kuhamisha kesi kama hizo kwa mahakama za kiraia.

Rais Museveni, hata hivyo, ameelezea kusikitishwa na uamuzi huo, akiutaja kuwa si sahihi na kuahidi kuupinga katika mahakama ingine.

Besigye ana historia ndefu ya mapambano na kisheria, ikiwa ni pamoja na mashtaka ya awali ya uhaini na ubakaji, ambayo amekuwa akisisitiza kuwa yalikuwa mambo ya kisiasa. Licha ya kuzuiliwa kwake, vyama vya upinzani vinadai kuwa utawala wa Museveni unazidi kutawaliwa na ukandamizaji wa kisiasa na kutovumilia ushindani kutoka kwa wapinzani.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved